January 22, 2019

Kwanini shule ya kwanza ya mtoto ni nyumbani?

Utakubaliana nasi kuwa shule ya kwanza katika maisha ya mtoto ni nyumbani – wazazi, ndugu wa familia tandaa, majirani na marafiki wa familia husika. Kupitia mzazi/mlezi mtoto anapata nyenzo zitakazoongoza maisha yake yote – heshima, utii, unyenyekevu na kadhalika. Yaani wema au ubaya wa mtu mara nyingi ni matokeo ya aliyojifunza nyumbani.   Nyumbani ndiko msingi hujengwa. Bahati nzuri ‘ualimu’ […]
January 18, 2019

#SimuliziZa116: Mtoto mfanyakazi za nyumbani aliyegeuzwa mke

Mama mmoja alitupigia simu namba 116 kutoa taarifa juu ya binti yake aliyekuwa amesafirishwa kutoka Songea kuja Dar es Salaam kufanya kazi kama #Mfanyakazi za nyumbani. ‘Nina wasiwasi sana juu ya maisha ya mwanangu, siwezi hata kulala vizuri siku hizi tangu siku niliyoambiwa kwamba sasa hafanyi tena kazi za nyumbani bali amegeuzwa mke wa mtu huko mjini.’ ‘Tafadhali nisaidieni.’ Aliongeza […]
January 15, 2019

Je mzazi unahusika katika kufaulu ama kufeli kwa mwanao masomoni?

Kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa watoto limekuwa tatizo kubwa katika jamii yetu. Pamoja na mambo mengi yanayochangia tatizo hili, kutokuwepo kwa ushirikiano kati ya walimu na wazazi katika kumlea mtoto kitaaluma ni kikwazo kikubwa ambacho makala hii itaangazia.   Wajibu na majukumu ya mzazi kwa mtoto wake anapokuwa nyumbani jioni baada ya shule (ama likizoni kwa wale wanaosoma shule […]
January 14, 2019

Je una malengo ya malezi ya mwaka mpya?

Tunapouanza mwaka mpya wengine tunaona kama Januari 2018 ilikuwa jana, si jambo la kushangaza namna muda unavyokwenda kasi. Ghafla unajikuta katika mwaka mwingine na watoto wanaongezeka kimo na umri kila mwaka. Je umejiwekea malengo gani ya malezi kwa mwaka ujao wa 2019? Kulea ni changamoto kwa kila mzazi, lakini siku hata siku tunajifunza kuwa wazazi bora zaidi ya jana! Tumekuwekea […]
December 17, 2018

Athari za Matumizi ya Vifaa vya Kielektroniki kwa Watoto

Kila mmoja wetu ni shahidi kwamba mabadiliko ya teknolojia yameleta athari hasi na chanya katika nyanja tofauti za maisha ya kila siku ya mwanadamu. Katika mabadiliko haya rika zote zimeguswa ikiwemo watoto. Watoto hufurahia matumizi ya vifaa vya kielektroniki kutokana na michezo (gemu) mbalimbali inayopatikana katika vifaa hivyo ikiwemo simu za mkononi, runinga na tablet. Pamoja na kwamba watoto hufurahia […]
December 11, 2018

Njia 7 za kumwepusha mtoto ‘kuharibikiwa’ msimu huu wa likizo

Inasikitisha kuona ingawa dhamira zetu ni nzuri kwa kuwapa watoto watakayo msimu huu, sisi wazazi ni sehemu ya tatizo pale watoto wanapoharibikiwa kadri wanavyokua. Tunakusogezea njia muhimu saba unazoweza kutumia kumwepusha mtoto kuharibikiwa. Mfundishe kuridhika. Mtoto akiridhika na alichonacho hawezi kutamani/kudai asivyonavyo. Mtoto wa umri wowote anaweza kujifunza kushukuru kwa zawadi aliopewa, kuridhika nayo na kuzoea kusema asante. Mtoto anayefahamu […]