May 17, 2017
Mtambulishe

Mtambulishe mtoto kwa wazazi na ndugu wa familia tandaa

Tamaduni zetu za kiafrika zinaasa malezi ya watoto kufanywa na wazazi wote wawili, mama na baba. Majira sasa yameanza kubadilika na leo si jambo la kushangaza kuona watoto wakilelewa na mzazi mmoja mara nyingi akina mama huku wakigombana na wenzi wao juu ya umiliki wa watoto kila mmoja akitaka kuchukua jukumu la kulea kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutengana kwa wazazi, […]
May 3, 2017
Kojoa

Jinsi ya kumsaidia mwanao aache kukojoa kitandani

Hata kama mwanao amefundwa na kuelewa kwamba anapobanwa na haja akahitaji kujisaidia lazima aende chooni, usishangae awapo usingizini hasa usiku bado akakojoa kitandani. Kukojoa kitandani ni jambo la kawaida hasa kwa watoto wenye umri chini ya miaka saba. Ifahamike kuwa kukojoa kitandani si jambo la hiari na hivyo halimpi mwanao fursa ya kulidhibiti. Kama ilivyo kuota jino la kwanza la […]
April 28, 2017
Uelewa

Namna 3 za kujenga uwezo wa mtoto kuelewa mambo

Wazazi wengi hupata fahari mtoto akitimiza umri wa miaka mitatu – baada ya shughuli nzito za kumuangalia akijifunza kukaa, kutambaa na sasa anamudu kutembea hata kuruka kama ‘mtu mzima! Anaonekana mjuzi wa mambo mengi si katika kutembea tu hata kuongea, kufanya maamuzi na ni rahisi kwa mzazi/mlezi kujisahau na kuanguka katika mtego wa kutarajia mengi zaidi kutoka kwake akidhani tayari […]
April 28, 2017
Thamini

Kuthamini matarajio ya mtoto sio kumdekeza

Matarajio ya watoto ni jambo ambalo limekuwa halipewi kipaumbele na wazazi ama walezi walio wengi kwa kudhani kwamba watoto ni viumbe wadogo wasio na fikra zenye mashiko. Makala haya yatazungumzia umuhimu wa mzazi kuyathamini matarajio ya mtoto na namna ambazo mzazi anaweza kufanikisha suala hili.   Ukiachilia mbali kwamba wazazi hudhani watoto hawawezi kuwa na mawazo chanya na yanayofikika, pia […]