June 2, 2019

Kwa nini tunapswa kuimarisha ulinzi wa watoto kuelekea siku kuu ya Iddi

Msimu wa sikukuu huambatana na furaha zisizo na kifani, furaha ambazo huwapunguzia wazazi uchovu unaotokana na mihangaiko yao katika kutafuta mkate wa kila siku. Furaha ambazo huiweka sawa miili na akili za watoto hususan mara baada ya kutoka masomoni na vilevile, furaha ambazo hujumuisha utolewaji na upokeaji wa zawadi kedekede miongoni mwa wazazi na watoto ndani ama nje ya familia. […]
May 30, 2019

Zijue adhabu zinazotolewazo sheria ya mtoto inapovunjwa

Makala haya yanaangazia baadhi ya adhabu chache zinazogusa maisha ya wazazi / walezi na hata watoto katika kutimiza majukumu yao ya kila siku. Ingawa adhabu zipo nyingi katika Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 ya Tanzania Bara, sisi tutakupa adhabu tatu kama ifuatavyo.   Mtoto anapopatikana na hatia. Sheria ya Mtoto inazuia mtoto kufungwa kifungo chochote kama vile vifungo vya […]
May 23, 2019

Kwanini mtoto aliye na umri wa chini ya miaka 10 hapaswi kupelekwa shule za bweni

Zipo sababu lukuki kwanini tunawapeleka watoto wetu shule za bweni ikiwa ni pamoja na kufiwa na wazazi wao, majukumu ya kusaka riziki kwa wazazi, elimu bora na zingine kadha wa kadha. Leo tutajadili athari za shule za bweni kwa watoto wenye umri mdogo. Umri wa chini ya miaka kumi na vipi elimu ya bweni inaweza kuwa ama chachu ya maendeleo […]
May 21, 2019

Fahamu sababu ya watoto wachanga kucheua

Kucheua kwa mtoto ni kitendo cha mtoto kutoa mabaki ya chakula yanayopitia mdomoni muda mfupi tu baada ya kula ama kunyonya. Kwa wazazi na walezi wengi, ni kitendo cha kawaida na mara nyingi baada ya mtoto kunyonya kauli kama ‘Mcheulishe mtoto,’ husikika.   Kucheua kwa mtoto hutokea mara baada ya mtoto kunyonya (ndani ya saa 1-2), watoto wachanga mathalan, wa […]
May 14, 2019

Hebu tuwalinde watoto dhidi ya unyanyasaji wa kingono mtandaoni

Mwaka 2018 zilipatikana takribani tovuti 105,000 zenye maudhui ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto. Tovuti hizi huwa na picha na video nyingi zinazoonesha watoto wakifanyiwa unyanyasaji kingono na kwa mwaka jana peke yake, zaidi ya picha 340,000 zilipatikana katika tovuti hizi na kuondolewa mtandaoni. Takwimu hizi zinatokana na ripoti ya Internet Watch Foundation, shirika linalofanya kazi ya kutafuta na kuondoa […]
April 25, 2019

#SimuliziZa116: Mtoto Salma asifirishwa toka Ngara na kutelekezwa barabarani Kilosa

Yalikuwa majira ya jioni kunako saa 1:35 usiku tulipopokea simu kutoka Kilosa mkoani Morogoro, Msamaria mwema atoa taarifa katika Kituo cha Huduma ya simu kwa mtoto kupitia namba 116 na kutanabaisha kuwa alimkuta msichana mwenye umri wa miaka 14 aliyejitambulisha kwa jina la Salma (Jina si halisi) kando ya barabara pindi alipokua njiani akitokea Morogoro mjini kuelekea Kilosa.Kimsingi, huu ulikua […]