February 25, 2019

Hizi hapa hatari tano anazoweza kukutana nazo mwanao mtandaoni.

Mara kadhaa kupitia wasaa huu tumezungumza juu ya matumizi ya mtandao na athari zake, chanya na hasi. Leo tunakutanabaishia aina tano kuu za hatari anazoweza kukutana nazo mwanao awapo mitandaoni na namna bora ya kukabiliana nazo ili kupafanya mtandaoni mahali salama kwa mwanao.   Maudhui yasiyofaa. Mtandaoni kuna maudhui chungu nzima kuanzia nyimbo za ibada hata filamu za utupu. Ingawa […]
February 11, 2019

Ujue waraka wa elimu kuhusu adhabu ya viboko shuleni Tanzania Bara

Kuvunjwa mikono, kuachwa na makovu mwilini pamoja na athari hasi za kiwango kikubwa zaidi kwa maana ya vifo ni matukio mbalimbali yaliyotendwa na yanayoendelea kutendwa dhidi ya wanafunzi mashuleni huku sababu kubwa ikihusisha adhabu ya viboko. Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, utolewaji wa adhabu hizo haufuati taratibu, kanuni pamoja na miongozo husika iliyowekwa.   Tunapenda kuwakumbusha wazazi, wanafunzi, walimu, […]
February 1, 2019

Hatupaswi kupata usingizi kwa watoto 10 waliochinjwa Njombe hapahapa Tanzania.

Matukio ya watoto wa umri kati ya miaka miwili hadi sita kuchinjwa na kukatwa koromeo, sehemu za siri na ulimi wilayani Njombe hapa-hapa Tanzania si ya kukalia kimya.   Hivi binadamu anatoa wapi ujasiri wa kumteka na baadae kumchinja mtoto wa miaka kati ya miwili hadi sita? Yaani unamkata koromeo, sehemu zake za siri, unanyofoa masikio alafu kama haitoshi unamtoa […]
January 25, 2019

Kwa nini mtoto anahitaji malezi ndani ya familia

Miaka ya hivi karibuni kumetokea mfumuko wa vituo vingi vya kulelea watoto waishio kwenye mazingira magumu. Hii ni kutokana na mfumo mzima wa malezi ya kifamilia kuingiwa doa na pia kuongezeka kwa vifo vya wazazi, ama kwa magonjwa (mfano Ukimwi), ajali za barabarani, nk. na kuacha watoto wengi yatima. Leo tuzungumze kuhusu malezi ya watoto wa ndugu na jamaa zetu […]
January 24, 2019

Athari za matumizi ya vifaa vya kielektroniki kwa watoto hizi hapa!

Kila mmoja wetu ni shahidi kwamba mabadiliko ya teknolojia yameleta athari hasi na chanya katika nyanja tofauti za maisha ya kila siku ya mwanadamu. Katika mabadiliko haya rika zote zimeguswa ikiwemo watoto. Watoto hufurahia matumizi ya vifaa vya kielektroniki kutokana na michezo (gemu) mbalimbali inayopatikana katika vifaa hivyo ikiwemo simu za mkononi, runinga na ‘tablets.’ Pamoja na kwamba watoto hufurahia […]
January 22, 2019

Kwanini shule ya kwanza ya mtoto ni nyumbani?

Utakubaliana nasi kuwa shule ya kwanza katika maisha ya mtoto ni nyumbani – wazazi, ndugu wa familia tandaa, majirani na marafiki wa familia husika. Kupitia mzazi/mlezi mtoto anapata nyenzo zitakazoongoza maisha yake yote – heshima, utii, unyenyekevu na kadhalika. Yaani wema au ubaya wa mtu mara nyingi ni matokeo ya aliyojifunza nyumbani.   Nyumbani ndiko msingi hujengwa. Bahati nzuri ‘ualimu’ […]