May 24, 2019

#SimuliziZa116: Baba asaini makubaliano kutoa matunzo kwa watoto baada ya talaka

Huduma ya Simu kwa Mtoto Zanzibar tulipokea simu kutoka kwa mama wa watoto watatu wenye umri wa miaka mitano (5), mitatu (3) na wa mwisho mwenye umri wa miezi kumi (10) pekee. Mama huyo mkazi wa shehia ya Dunga, wilaya ya Kati Unguja na alipiga simu kutoa lalamiko kwamba mumewe wa zamani ametelekeza wajibu wa kuwalea watoto wao.   ‘Ni […]
May 23, 2019

Kwanini mtoto aliye na umri wa chini ya miaka 10 hapaswi kupelekwa shule za bweni

Zipo sababu lukuki kwanini tunawapeleka watoto wetu shule za bweni ikiwa ni pamoja na kufiwa na wazazi wao, majukumu ya kusaka riziki kwa wazazi, elimu bora na zingine kadha wa kadha. Leo tutajadili athari za shule za bweni kwa watoto wenye umri mdogo. Umri wa chini ya miaka kumi na vipi elimu ya bweni inaweza kuwa ama chachu ya maendeleo […]
May 23, 2019

#SimuliziZa116: Mume aripoti kubakwa mkewe, mke akataa kortini.

Kituo cha Huduma ya Simu kwa Mtoto kilipokea simu kutoka baba mmoja ambaye aliripoti kwamba mke wake amebakwa. Mhalifu ambaye alikuwa akiendesha gari alipaki na kuomba kujisaidia nyumbani kwao na baada ya kumaliza haja yake alipata kusikia mazungumzo ya mke na mume kuhusu kwenda sokoni na akapendekeza kumpa mke lifti kwani alikuwa anaelekea njia hiyohiyo.   Njiani alimuomba mama mwenye […]
May 21, 2019

Fahamu sababu ya watoto wachanga kucheua

Kucheua kwa mtoto ni kitendo cha mtoto kutoa mabaki ya chakula yanayopitia mdomoni muda mfupi tu baada ya kula ama kunyonya. Kwa wazazi na walezi wengi, ni kitendo cha kawaida na mara nyingi baada ya mtoto kunyonya kauli kama ‘Mcheulishe mtoto,’ husikika.   Kucheua kwa mtoto hutokea mara baada ya mtoto kunyonya (ndani ya saa 1-2), watoto wachanga mathalan, wa […]
May 14, 2019

Hebu tuwalinde watoto dhidi ya unyanyasaji wa kingono mtandaoni

Mwaka 2018 zilipatikana takribani tovuti 105,000 zenye maudhui ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto. Tovuti hizi huwa na picha na video nyingi zinazoonesha watoto wakifanyiwa unyanyasaji kingono na kwa mwaka jana peke yake, zaidi ya picha 340,000 zilipatikana katika tovuti hizi na kuondolewa mtandaoni. Takwimu hizi zinatokana na ripoti ya Internet Watch Foundation, shirika linalofanya kazi ya kutafuta na kuondoa […]
April 30, 2019

Mtoto Josephine (jina halisi limehifadhiwa) atolewa katika ndoa na kurudi shuleni.

Mnamo tarehe 10 Januari mwaka 2019 jirani mmoja kutoka wilayani Hai kata ya Bondeni alipiga simu Kituo cha Huduma ya Simu kwa Mtoto kupitia namba 116 na kutoa taarifa zilizomhusu binti wa miaka 12 aliyetambulika kwa jina la Josephine. Jirani huyo alieleza kuwa, Josephine alifanikiwa kumaliza darasa la saba mnamo mwaka 2018 na matokeo yalivyotoka akafanikiwa kupata ufaulu mzuri wa […]
escort | bayandanalhaberi.com