March 6, 2019

Kwa nini mwalimu aliyemchapa mtoto hadi kufa amehukumiwa kunyongwa

Marehemu alikuwa anasoma wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kibeta iliyoko Manispaa ya Bukoba, jina lake ni Sperius Eradius amefariki akiwa na miaka 13, baada ya kipigwa na mwalimu wake akituhumiwa kuiba pochi ya mwalimu.   Siku ya tukio marehemu Sperius Eradius alikwenda kumpokea mizigo mwalimu wake aliyefika shuleni hapo kwa usafiri wa bodaboda, lakini baada ya mwalimu […]
February 26, 2019

#SimuliziZa116: Aolewa na alombaka kuficha aibu ya familia (muhali)

Mnamo Februari 14, 2019, Huduma ya Simu kwa Mtoto Unguja tulipokea simu kutoka kwa binti akiomba msaada kulipa bili ya matibabu ya mtoto wa kiume wa dada yake ambaye amekuwa akiugua kwa miezi takribani 10 sasa. Mtoto huyo alizaliwa na tatizo la kuvuja kwa mkojo ndani ya mwili – tatizo linalomsumbua mpaka leo.   Binti huyo alitupa kisa cha namna […]
February 25, 2019

Hizi hapa hatari tano anazoweza kukutana nazo mwanao mtandaoni.

Mara kadhaa kupitia wasaa huu tumezungumza juu ya matumizi ya mtandao na athari zake, chanya na hasi. Leo tunakutanabaishia aina tano kuu za hatari anazoweza kukutana nazo mwanao awapo mitandaoni na namna bora ya kukabiliana nazo ili kupafanya mtandaoni mahali salama kwa mwanao.   Maudhui yasiyofaa. Mtandaoni kuna maudhui chungu nzima kuanzia nyimbo za ibada hata filamu za utupu. Ingawa […]
February 11, 2019

Ujue waraka wa elimu kuhusu adhabu ya viboko shuleni Tanzania Bara

Kuvunjwa mikono, kuachwa na makovu mwilini pamoja na athari hasi za kiwango kikubwa zaidi kwa maana ya vifo ni matukio mbalimbali yaliyotendwa na yanayoendelea kutendwa dhidi ya wanafunzi mashuleni huku sababu kubwa ikihusisha adhabu ya viboko. Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, utolewaji wa adhabu hizo haufuati taratibu, kanuni pamoja na miongozo husika iliyowekwa.   Tunapenda kuwakumbusha wazazi, wanafunzi, walimu, […]
February 1, 2019

Hatupaswi kupata usingizi kwa watoto 10 waliochinjwa Njombe hapahapa Tanzania.

Matukio ya watoto wa umri kati ya miaka miwili hadi sita kuchinjwa na kukatwa koromeo, sehemu za siri na ulimi wilayani Njombe hapa-hapa Tanzania si ya kukalia kimya.   Hivi binadamu anatoa wapi ujasiri wa kumteka na baadae kumchinja mtoto wa miaka kati ya miwili hadi sita? Yaani unamkata koromeo, sehemu zake za siri, unanyofoa masikio alafu kama haitoshi unamtoa […]
January 31, 2019

#SimuliziZa116 – ulawiti katika kituo cha kulelea watoto

Jirani msamaria mwema alipiga simu namba 116 Kituo cha Huduma ya Simu kwa Mtoto baada ya kushuhudia tendo la ulawiti katika kituo cha kulelea watoto kilichopo jirani na makazi yake. Aliendelea kusimulia kuwa, mwanaume mtu mzima aliekadiriwa kuwa na umri wa miaka takriban 40 ama zaidi ambaye kimsingi ni mlezi wa watoto katika kituo hicho alimlawiti mtoto wa miaka 13 […]