News

#Mfanyakazi: mradi wa kutokomeza usafirishaji haramu wa watoto wazinduliwa

Last updated 3 years ago

#Mfanyakazi: mradi wa kutokomeza usafirishaji haramu wa watoto wazinduliwa

Shirika la C-SEMA limetambulisha mradi mpya uitwao ‘MFANYAKAZI’ hapa mkoani Singida wenye bajeti ya TZS. 53,000,000. Mradi huu utatekelezwa kwa mwaka mmoja kuanzia Julai 2020 mpaka Juni 2021. Lengo kuu la mradi huu ni kutokomeza biashara haramu ya usafirishaji haramu wa watoto kwa ajili ya kuwatumikisha sambamba na utekelezaji wa mpango kazi wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na Watoto (MTAKUWWA) 2017 – 2022)

Afisa ustawi wa mkoa wa Singida Bi. Shukrani Mbago akiwakaribisha washiriki na wadau kutoka C-SEMA alisema mradi huu utasaidia sana katika jitihada za serikali katika mkoa wa Singida haza katika utekelezaji wa MTAKUWWA (2017-2022)

Mkurugenzi wa Huduma ya Simu kwa Mtoto na Mkuu wa Miradi kutoka shirika la C-SEMA Ndugu Michael Marwa aliwashukuru uongozi wa mkoa kwa kuratibu na kupokea ombi la kutekeleza mradi wa #Mfanyakazi hapa Singida.

Akizumgumza wakati wa kutambulishwa kwa mradi huo Kaimu Katibu Tawala Msaidizi (Afya) Mkoa wa Singida Ndugu Ernest Mgeta aliwapongeza wawakilishi wa shirika la C-SEMA na kuahidi kupata ushirikiano katika utekelezaji wa mradi wa 'MFANYAKAZI'.

Mradi wa #Mfanyakazi utazingatia kuimarisha uwezo na uhusiano kati ya wasimamizi wa ulinzi wa Watoto Halmashauri ya wilaya ya Singida katika kugundua, kuzuia, na kushughulikia matukio ya biashara haramu ya usafirishaji haramu wa watoto mkoani Singida na kujenga  ufahamu juu ya suala hili kwa watoto na wanajamii wote ili kupunguza au kutokomeza vitendo hivyo.

Malengo haya yatafikiwa kwa kufanya kazi shuleni kwa kuzungumza na Watoto, kuwajengea uwezo na kuwahamasisha kuripoti na kutoa taarifa za udhalilishaji na ukatili wanaofanyiwa. Pia Shirika la C-SEMA litafanya vipindi vya redio ili kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu tatizo hili. Mradi huu pia utawajengea uwezo watumishi na wadau wanaounda kamati za ulinzi wa wanawake na Watoto katika Halmashauri ya wilaya ya Singida ili kuimarisha mfumo wa ulinzi wa Watoto mkoani Wilayani hapo. Ni matarajio ya mradi kuwa jamii itahamsika na kuripoti matukio yote ya biashara haramu ya usafirishaji haramu wa wa watoto kwa ajili ya kutimikshwa kwa kupitia namba ya huduma ya simu kwa mtoto ya (116).