Tumetoka kuadhimisha Siku ya Afya ya Akili Duniani, na sasa ni wakati mwafaka kuzungumzia jinsi wazazi wanaweza kujinusuru na uchovu uliopitiliza utokanao na pilika za kulea watoto, maarufu kama “parental burnout.”
Kama tunavyojua, malezi ya watoto ni moja ya jukumu lenye furaha kubwa, lakini linahitaji nguvu nyingi. Matarajio ya kuwa mzazi anayepatikana kila wakati kwa watoto wetu, mvumilivu, na mwenye huruma yanaweza kuwa changamoto kubwa kwa sababu,wazazi wengi tunajaribu kumudu utafutaji wawa kipato, majukumu ya nyumbani, pamoja na kuhakikisha kwamba mahitaji ya kihisia na kimwili ya watoto wetu yanazingatiwa. Katika kufanya hivi, tunaweza kukuta wiki auau hata mwezi umepita bila sisi kupumzika vizuri. Ingawa ni kawaida kuhisi uchovu mara kwa mara, lakini aina ya uchovu tunaouzungumzia leo, ni ule uliopitiliza ("parental burnout") ambao ni hali ya tofauti kabisa.
Makala hii inaangazia sababu, dalili, na mbinu za kujinasua na uchovu wa wa aina hiyoo kwa wazazi, kwa kuzingatia tafiti tofauti za kisaikolojia na sayansi.
Uchovu wa kulea 'parental burnout' ni nini?
Parental burnout sio tu uchovu wa kawaida baada ya siku ndefu. Ni hali ya uchovu mkubwa wa kihisia, kujitenga na watoto kihisia, na kupoteza hamu ya kuwa mzazi au kutekeleza jukumu la malezi. Kwa mujibu wa Dkt. Isabelle Roskam, mtafiti maarufu wa mada hii, uchovu huu una vipengele vitatu vikuu:
Uchovu wa kihisia.
Kujitenga kihisia na watoto.
Kujiona huwezi kutekeleza vizuri majukumu yako kama mzazi.
Tofauti na uchovu wa kawaida, hali hii huleta umbali wa kihisia kati ya mzazi na mtoto, hali inayosababisha ugumu wa kuwa na upendo na uvumilivu katika safari ya malezi.
Sababu za uchovu wa wazazi
Sababu kadhaa huchangia uchovu huu. Utafiti uliochapishwa kwenye Jarida la Ndoa na Familia unaonesha kuwa uchovu huu uliopitiliza parental burnout kwa wazazi hutokeauongezeka pale wanapohisi wanakosa usawa kati ya majukumu ya kibinafsi na yale ya malezi. Mawazo ya kuwa mzazi kamili, hasa kutokana na kujilinganisha na wazazi wengine kupitia mitandao ya kijamii, linazidi kuleta changamoto za kihisia na kimwili kwa wazazi.
Aidha, tabia zetu wenyewe zinaweza kuongeza hatari ya kupata uchovu wa kulea. Wazazi wanaojitahidi kufikia ukamilifu (perfectionists), ambao hujiwekea matarajio yasiyo ya kweli, wanakumbwa na hisia za kuzidiwa wanapokutana na changamoto za malezi. Vilevile, ukosefu wa msaada kutoka kwa familia na ndugu wa karibu umeonekana kuchangia dalili za aina hii ya uchovu parental burnout, ambapo wazazi wanaohisi wapweke wanakuwa katika hatari zaidi.
Dalili za aina hii ya uchovu parental burnout ni pamoja na kujisikia kuchoka hata baada ya kupumzika, kujitenga kihisia kwa kushindwa kujenga ukaribuungana ‘bond’ na watoto na kujihisi kama tunatekeleza majukumu ya malezi kwa mazoea bila furaha pamoja na kushindwa kutimiza majukumu ya yetu kama wazazi hata pale tunapojitaidi kwa nguvu zote.
Wazazi wanaopitia hali hii ya parental burnout pia wanakuwa wakali zaidi au wanaweza kuwa na hasira za ghafla, hali ambayo huwaogopesha watoto na pengine kuweza kuwaweka hatarini huku uchovu ukizidi kushika hatamu kwa wazazi.
Uzuri ni kwamba Uchovu huu uliopitiliza na kusababisha msongo wa mawazo kwa mzazi parental burnout unatibika. Dkt. Moïra Mikolajczak, mtaalamu wa saikolojia, anapendekeza mikakati ifuatayo ya kuuponya:
Tutambue pale tutakapokua tumechoka kupitiliza tukizingatia dalili tulizozitaja hapo awali. Mara nyingine wazazi huwa tunaogopa kukiri kwamba tunahitaji msaada katika malezi. Lakini hata hivyo, kutambua wazi kwamba tunapitia tatizo la uchovu wa kulea parental burnout ni hali halisi ya kisaikolojia inayoweza kuwa hatua ya kwanza kuelekea kupona.
Tuweke mipaka ya kuomba msaada, hakuna mzazi anayeweza kufanya kila kitu peke yake. Ni muhimu kuweka mipaka halisi na kuomba msaada kutoka kwa wenza wetu, familia na marafiki zetu, au wataalamu wa saikolojia na hata kupitia huduma zilizopo za watoto mfano huduma ya simu kwa watoto 116. Kusaidiana kunatupa faraja ya kufahamu kwamba hatupo peke yetu na kutupa nguvu ya kuendelea.
Vile vile ni muhimu sana kuchukua muda wa kupumzika peke yetu, huu sio ubinafsi bali ni jambo la lazima. Utafiti unaoneshayesha kuwa hata vitendo vidogo vya kujitunza, kama kutembea, kutafakari, kusoma vitabu, kulala, au kufanya mambo tunayoyapenda, vinaweza kupunguza dalili za uchovu huuparental burnout. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Mikolajczak et al. (2018), wazazi wanaojihusisha na shughuli za kujitunza, hata kwa muda mfupi, huonyesha dalili ndogo za uchovu wa kihisia na kisaikolojia, ikilinganishwa na wale ambao hawachukui muda wa kujitunza.
Utafiti huo ulionyesha kuwa kujipa muda wa mapumziko na kufanya vitu vya kufurahisha kunaongeza ustawi wa kiakili na kimwili kwa wazazi, na kuwafanya wawe na nguvu na uvumilivu zaidi katika majukumu ya Malezi.
Pia, tujitahidi kupanga upya majukumu yetu ya kila siku na kuweka kipaumbele kwa vitu muhimu. Hii itatusaidia kuepuka kukumbwa na kazi nyingi kupita kiasi. Muda wa kupumzika ni lazima.
Ikiwa hali ya uchovu wa kulea 'parental burnout' inaendelea, tunashauriwa kutafuta tiba au ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu wa kisaikolojia. Kwa wazazi wa kitanzania, hili ni jambo geni lakini tiba ya kitabia ya kiakili (CBT) imeonesha kusaidia wazazi wengi kubadilisha mtazamo wao juu ya visabibishi vya uchovu wa kulea na kuwasaidia kupona kwa uharaka na kuendelea kuishi kwa namna ya utulivu hata pale chagamoto za maisha zikiwakabili.
Tufahamu kwamba, parental burnout ni hali halisi inayotambuliwa kisayansi, na huathiri wazazi wengi kote duniani. Hivyo tuwe makini, tujitahtmini kiundani na tuchukue hatua za kutunza afya zetu za akili,kama lengo letu ni kuwa walezi bora kwa watoto wetu.
Kwa maoni na ushauri, tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozwi malipo kutoka mitandao yote nchini. Vilevile, unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook, Twitter na Instagram: @SemaTanzania.