top of page
  • C-Sema Team

#SimuliziZa116: ulawiti katika kituo cha kulelea watoto


Jirani msamaria mwema alipiga simu namba 116 Kituo cha Huduma ya Simu kwa Mtoto baada ya kushuhudia tendo la ulawiti katika kituo cha kulelea watoto kilichopo jirani na makazi yake. Aliendelea kusimulia kuwa, mwanaume mtu mzima aliekadiriwa kuwa na umri wa miaka takriban 40 ama zaidi ambaye kimsingi ni mlezi wa watoto katika kituo hicho alimlawiti mtoto wa miaka 13 kituoni hapo. Kitendo hicho cha kidhalimu kiliteka hisia za jirani huyo na kushindwa kuvumilia na ndipo alipoamua kupiga simu namba 116 kupata msaada.


Tulipokea taarifa hizo na kuzifikisha kwa Afisa Ustawi wa Jamii Temeke ambaye mara moja alianza uchunguzi wa kina juu ya swala hili akishirikiana na Dawati la Jinsia na Watoto la Polisi. Uchunguzi ulibaini kuwa matukio ya kulawiti watoto kituoni hapo yamekithiri na hivyo jalada lilifunguliwa kumshitaki mtuhumiwa.


Mpaka sasa, afya ya mtoto imeimarika vyema ingawa kwa bahati mbaya, mhusika wa tukio hilo alitoroka na hivyo hajafikishawa mahakamani. Hata hivyo, polisi wanaendelea kufanya jitahada kubwa kila iitwapo leo ili waweze kumtia nguvuni mtuhumiwa. Aidha, kituo cha huduma ya simu kwa mtoto kinaendelea kusuburi taarifa za mara kwa mara juu ya muendelezo wa kesi hiyo kutoka kwa Afisa-Ustawi pamoja na Dawati la Jinsia la Polisi kwa madhumuni ya kupatikana kwa haki za watoto wa kituo hicho.


Tusikae kimya tukijua matukio kama haya yanaendelea mitaani na vitongojini mwetu. Wasiliana nasi kupitia nambari 116 bila malipo tuzungumze.

0 views

Comments


bottom of page