Stories

Asilimia 80 ya malezi ni mahusiano yaliyopo kati yako na mtoto wako

Last updated 2 months ago

Asilimia 80 ya malezi ni mahusiano yaliyopo kati yako na mtoto wako

Laura Markham, mwanaharakati wa #Malezi anasema kwamba asilimia 80 ya malezi ni mahusiano yaliyopo kati yako na mtoto wako na asilimia 20 ni unavyo mwongoza. 

Anamaanisha kwamba watoto watakusikiliza na kufuata unachowaambia vizuri kama mahusiano yenu ni mazuri. 
Hata sisi watu wazima aina ya mahusiano yetu na watu yanaashiria namna gani tunawasikiliza.

Kumuongoza mtoto katika maisha yake ni kitu chema Ila tusisahau kuwekeza katika mahusiano yetu nao.

Tunasisitiza kuwa; 

-Msikilize mtoto kwa ‘umakini’ akiwa anakuongelesha. 

-Mkubali mtoto wako kama alivyo na jaribu kudhibiti matarajio yako kwake.

-Jenga uaminifu na mtoto kwa kuwa na maongezi nae mara kwa mara, timiza ahadi zako kwake na mpongeze akifanikiwa.

- Mfundishe kuomba msamaha akikosea kwa kumuomba msamaha ukimkosea (anajifunza kwako) 

Malezi yanahitaji malengo na uvumilivu wa kutimiza malengo hayo. Hivyo kama lengo lako ni kuwa na mahusiano mema na mtoto wako weka juhudi, unaweza!