Stories

Ujauzito baada ya umri wa miaka 35.

Last updated one year ago

Ujauzito baada ya umri wa miaka 35.

Kuna msemo usemao, ‘umri si chochote isipokuwa ni namba tu.’ Lakini linapokuja suala la ujauzito na kupata mtoto mwenye siha njema, umri unahusu. Ni kweli kwamba kuna wanawake wengi ambao wana umri wa kuanzia miaka 35 au 40 na zaidi na bado wamepata watoto wenye siha njema. Hata hivyo haimaanishi kwamba usichukue tahadhari katika kuboresha afya yako na ya mwanao na kuepuka hatari zinazotokana na kupata ujauzito ukiwa na umri wa miaka 35 na zaidi. Mama mjamzito mwenye umri wa miaka 35 au zaidi anakuwa na hatari kubwa ya kupata mtoto mwenye dosari za maumbile.

Nawezaje kuongeza uwezekano wa kupata mtoto mwenye siha (afya) njema?

Kupata ushauri na vipimo kabla ya kushika ujauzito. Unapoamua kwamba uko tayari kupata mtoto, ni muhimu kuzingatia baadhi mambo yafuatayo kabla ya kupata ujauzito.

Mwone daktari wako kwa uchunguzi ili kuona kama una afya stahiki kabla ya kushika ujauzito. Ongea nae kuhusu utayari wako wa kiakili na kimwili kwa ajili ya kupokea ujauzito.

Fanya uchunguzi wa mara kwa mara na wa mapema katika kipindi chote cha ujauzito. Miezi miwili ya kwanza ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya mwanao. Uchunguzi wa mapema na wa mara kwa mara huongeza uwezekano wa kupata mtoto mwenye siha (afya) njema Baadhi ya vitu vinavyofanyika katika kipindi hiki cha ujauzito (kliniki) ni pamoja na vipimo kwa ajili ya uchunguzi wa afya ya mama na mtoto aliye tumboni, elimu ya afya ya mama na mtoto, ushauri na kutiana moyo.

Kupata huduma za kliniki kwa mama mjamzito husaidia kuchukua tahadhari kwa mama mjamzito na humsaidie mama aliye na umri wa miaka 35 na zaidi kujipanga vyema kupata mtoto. Humsaidia daktari wako kuyajua matatizo yanayowapata akina mama wajwazito na hasa walio na umri miaka 35 na zaidi.

Mathalani akina mama hawa huwa wanakuwa kwenye hatari ya kupata kisukari au prieklampsia (preeclampsia – hali inayochagiza kupata kifafa cha mimba), ugonjwa wa shinikizo la damu la juu linaloambatana na protini kwenye mkojo. Katika kipindi cha kutembelea kliniki daktari wako akatupima shinikizo la damu, protini kwenye mkojo na atakupima kuona kama una kisukari cha ujauzito. Hivyo kama kuna tatizo katika kipindi cha ujauzito litaonekana mapema na kushughulikiwa.

Kumbuka upimaji wa vipimo vingine kwa mama mjamzito aliye na umri wa miaka 35 au zaidi. Daktari wako atakuandakia vipimo maalumu kwa ajili ya akina mama wajawazito watu wazima. Vipimo hivi vitakusaidia kuweza kutambua kama uko kwenye hatari ya ya kupata mtoto mwenye dosari ya maumbile. Muulize daktari wako kuhusu faida na hasara za kufanya vipimo hivi ili uweze kufanya uamuzi sahihi.

Tumia vidonge vinavyotumiwa katika kipindi cha ujauzito. Wanawake wote wa walio katika umri wa kuzaa wanatakiwa kutumia vidonge vya foliki mikrogramu 400 kila siku. Kupata vidonge vya foliki kila siku na baada ya miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito inaweza kusaidia kama kinga dhidi ya dosari za maumbile kama vile mgongo wazi au dosari katika ubongo wa mtoto. Matumizi ya vidonge vya foliki hutoa safu ya ulinzi kwa wanawake wenye umri umri mkubwa (miaka 35 na zaidi) ambao ndio walio na hatari ya kupata watoto wenye watoto wenye dosari ya maumbile. Baadhi ya vidonge vya foliki huwa na mikrogramu 800-1,000. Bado pia navyo ni salalma kwa ujauzito.

Ukweli ulivyo ni kwamba, baadhi ya wanawake huhitaji na mikrogramu zaidi ya 400 kwa ajili ya ulinzi wa dosari kwenye maumbile ya vichanga tarajiwa. Usitumie zaidi ya mikrogramu 1,000 (miligramu moja) za vidonge vya foliki bila ya kutafuta ushauri toka kwa daktari wako. Kumbuka wanawake wenye dosari za maumbile huhitaji mikrogramu 4,000 za vidonge vya foliki.

Nawezaje kushusha hatari ya kupata ujauzito wenye matatizo?

Unastahili matunzo, mapenzi na uangalizi sawa na ya mtoto wako tarajiwa. Huduma hizi zitakusaidia kudhibiti matatizo ya afya unayoweza kuwa nayo na kukukinga dhidi ya kisukari cha ujauzito  pamoja na shinikizo la damu la juu. Kadri utakavyokuwa na afya njema ndivyo atakavyokuwa na mwanao.

Usije ukapuuzia miadi na madaktari wengine kama una tatizo la kitabibu la kudumu kama kisukari au au shinikizo la damu la juu. Kamwe usisahau ratiba ya miadi ya magonjwa yako ya kudumu. Kumbuka kushughulikia magonjwa yako ya kudumu kabla ya kupata ujauzito kutasaidia kukuweka wewe na mwanao katika siha njema na kuepuka maudhi yanayowaandama wajawazito wengi.

Kumbuka kumtembelea dakatri wako wa meno kwa ajili ya uchunguzi. Kuwa meno na fizi zenye afya hupunguza uwezekano wa kujifungua kabla ya wakati pia hupunguza uwezekano wa kupata watoto njiti.

Dumisha lishe bora na iliyo na uwiano mzuri. Kula vyakula vya aina tofauti tofauti kutakusaidia kupata virutubisho vyote unavyohitaji. Kila siku tumia mboga za majani na matunda ya aina mbalimbali, nafaka kamili (unga usiokobolewa, n.k.), maharage, pamoja na maziwa machundu ikiwa ni pamoja na vayakula vingine vilivyo na ukwasi mwingi wa madini ya kalisi (calcium). Kwa njia hiyo utaweza kudumisha afya ya meno na mifupa yako mwenyewe na kumsaidia mwanao kuendelea kukua kwa afya njema.

Pia usisahau kujumuisha vyakula kama vile mboga za majani, maharage makavu, maini na baadhi ya matunda ya jamii ya sitrusi kama vile machungwa, ndimu na n.k. kwani hivi vina kiwango kizuri cha madini ya foliki.

Kuwa na kiwango cha uzito kinachotakiwa. Ongea na daktari wako kujua ni kiasi cha gani cha uzito kinachohitajika katika kipindi hiki cha ujauzito. Wanawake wenye BMI ya kawaida wanatakiwa kuongeza uzito wa kilogramu 1 mpaka 15.  Kama tayari ulikuwa na uzito mkubwa kabla ya kuwa mjamzito daktari wako anaweza kupendekeza uongeze kati ya kilogramu 6 na 11. Kuwa na uzito muafaka kutakusaidia kupunguza uwezekano wa kupata mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati. Pia utapunguza hatari ya kupata kisukari katika kipindi cha ujauzito au shinikizo la damu la juu la kipindi cha ujauzito.

Fanya mazoezi ya mara kwa mara. Mazoezi ya mara kwa mara yatakusaidia kuwa na uzito muafaka katika kipindi hiki cha ujauzito. Kufanya mazoezi huku kutakupatia nguvu na kukuepusha na msongo. Kumbuka wewe na daktari wako katika kipindi hiki mnaweza kupitia upya programu yako ya mazoezi. Kuna uwezekano mkubwa unaweza ukaendelea mazoezi mengi tu kama unatakavyoshauriwa na daktari. Daktari wako atakusaidia ni mazoezi gani utaendelea nayo na mazoezi gani unahitaji kupunguza, n.k.

Sitisha kuvuta sigara au kutumia kileo. Hutakiwi kuvuta sigara au kutumia kileo katika kipindi chote cha ujauzito. Matumizi ya pombe yatamuweka mwanao katika hatari ya kupata hitilafu katika akili na katika viungo vya mwili. Uvutaji wa sigara nao huongeza uwezekano wa kujifungua mtoto mwenye uzito pungufu ambalo ni tatizo linalowakumba zaidi wajawazito watu wazima (miaka 35 na zaid). Kutokuvuta sigara kunasaidia kukukinga na prieklampsia (hali inayopelekea kupata kifafa cha mimba).

Muulize daktari wako kuhusu dawa unazohitaji kutumia wakati wa ujauzito iwapo ulikuwa unavuta sigara kabla ya ujauzito. Muulize dakatari wako kuhusu ni dawa gani zilizo salama kutumia ukiwa unanyonyesha ili kumjengea mtoto wako kinga. Mweleze daktari historia ya dawa ulizotumia ulizoandikiwa na daktarai na hata zile unazotumia bila ya kuandikiwa na dakatari, virutubisho na dawa za miti shamba. Ajue namna ya kukusaidia.

Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116 ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, Instagram @sematanzania na www.sematanzania.org