Stories

Yajue madini na vitamini muhimu wakati wa ujauzito.

Last updated one year ago

Yajue madini na vitamini muhimu wakati wa ujauzito.

Ujauzito na vitamini zinazotolewa wakati wa ujauzito.

Ni vitamini gani zinatumika katika kipindi cha ujauzito?

Katika kipindi cha ujauzito kula chakula chenye uwiano wenye lishe bora ni jambo la msingi sana. Pia ni jambo la msingi kutumia vitamini katika kipindi cha ujazuzito ili kuziba pengo la upungufu wa virutubisho linaloweza kujitokeza katika lishe ya mama mjamizito katika kipindi cha ujauzito.

Virutubisho vinavyotumika katika kipindi cha ujauzito vina madini megi na vitamini ambazo zinahitajika katika kipindi cha ujauzito, ikiwemo madini ya kalisi (calcium) yaliyo muhimu sana kwa mjamzito.

Madini ya chuma, kalisi (calcium) na foliki asidi.

Vidonge vya foliki asidi husaidia katika kukinga dhidi ya dosari katika neva za fahamu na hivyo kuepusha doasri za kimaumbile katika ubongo na katika uti wa mgongo.

Dosari katika neva za fahamu huanza kutokea katika siku 28 za kwanza baada ya kutungwa kwa mimba, kabla hata ya mama kujua kuwa ni majamzito. Tafiti zinaonesha nusu ya mimba zote hazikuwa zimepangwa hivyo inapendekezwa kuwa mwanamke yeyote anayetarajia kupata ujauzito atumie mickrogrmu 400 za vidonge vya foliki asidi kila siku, akianza kabla ya kupata ujauzito na kuendelea namna hiyo kwa wiki 12 za ujazito. Muda huu wa wiki 12 za mwanzo wa ujauzito ndiyo muda ambao ubongo na mfumo wa neva unajengwa na kukua.

Mama ambaye tayari amepata mtoto mwenye dosari katika neva za nyuroni (mfumo wa fahamu) anahitaji ajadiliane na daktari wake kama atahitaji vidonge vya foliki na dozi yake itakuwa ni ipi. Tafiti zinaonesha kwamba matumizi ya mikrogramu 4,000 kwa mwezi mmoja kabla na katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo wa ujauzito zinaweza kusaidia kutatua tatizo hili. Tafadhali usitumie dawa hizi mwenyewe bila kujadiliana na daktari kwanza.

Vyakula vilivyo na foliki asidi katika kiwango kiubwa ni kama mboga za majani kibichi, njugu (karanga, njugumawe, nazi, korosho, n.k.) maharage, matunda ya jamii ya sitrusi ambayo ni kama machungwa, ndimu, machenza na n.k. bila kusahau vyakula vilivyoongezewa foliki asidi. Hata hivyo usisahau kuwa virutubisho ni nyongeza tu na vinatakiwa vitumiwe katika kiwango sahihi. Shauriana na daktari wako matumizi sahihi.

Madini ya kalisi (calcium) nayo ni muhimu kwa mama mjamzito kwani husaidia katika ukuaji wa mifupa ya mtoto na kumkinga mtoto dhidi ya upotevu wa ujazo wa mifupa yake (bone density).

Madini joto ama aidini (iodine) ni muhimu kwa ajili ya afya na ukuaji wa mtoto katika kipindi cha ujauzito. Upungufu wa madini joto (iodine) katika mwili wa mama unaweza kusababisha kudumaa kwa mtoto, utahiira na hata uziwi kwa mtoto. Upungufu wa madini haya unaweza kusababisha kuzaa mtoto mfu au mimba kutoka.

Madini ya chuma (iodine) husaidia kubeba hewa ya oksijeni kwa mama na kwa mtoto aliyeko tumboni.

Zingatia matumizi ya vitamini na madini yenye dozi hizi unapokuwa ukitafuta virutubisho vya kutumia katika kipindi cha ujauzito: -

Mikrogramu 400 za foliki asidi.

 I U 400 IU za vitamini D.

 Miligramu 200 mpaka 300 za madini ya kalisi (calcium).

Miligramu 70 za vitamini C.

Miligramu 3 za vitamini B₁ (thiamine).

Miligramu 2 za vitamin B₂ (riboflavin).

Miligramu 20 za vitamini B3 (niacin).

Mikrogramu 6 za vitamini B12.

Miligramu 10 za vitamini E.

Miligramu 15 za zinki.

Miligramu 17 za madini ya chuma (iron).

Mikrogramu 150 za madini joto (iodine).

Vilevile kwa kuzingatia uzoefu na vipimo, daktari anaweza kukuandikia baadhi tu ya vitamini zinazohitajika katika kipindi cha ujauzito na kukupunguzia ulazima wa kutumia aina zote tajwa hapo juu za vitamini na madini.

Vipi iwapo vitamini na dawa hizi zitakuletea kichefuchefu?

Baadhi ya vitamini zinaweza kuleta kichefuchefu kwa mama mjamzito ambaye kwa kawaida huwa tayari ana kichefuchefu. Endapo hili litatokea muone mtaalamu wa afya. Yeye ataweza kukuandikia aina tofauti za vitamini ili kukupunguzia hali ya kichefuchefu mathalani baadhi ya wajawazito wanaweza wakatumia bila shida vitamini za kutafuna, kumeza na wengine za kunywa huwa zinawafaa zaidi.

Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116 ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, Instagram @sematanzania na www.sematanzania.org